Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mheshimiwa Iddi Kimanta amepokea misaada ya kupambana na ugonjwa wa Covid_19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Msaada wa kwanza umetolewa na Chuo Kikuu cha Dar-es- Salaam kupitia Taasisi yake ya Tanzania Partnership Programme(TPP) inayofanya shughuli zake katika Kata ya Mswakini .
Vifaa vilivyotolewa ni;Chlorine Kilo 108,Sanitizer Lita 35,Gloves1500,Sagical Mask 800 na Vipima joto 3.
Akikabidhi Vifaa hivyo Msimamizi wa Programu Nd.Jonathan Simon amesema TPP imeamua kuunga Mkono juhudi za kupambana na ugonjwa wa Covid_19 baada ya kuona kuwa uhitaji Mkubwa wa vifaa tiba na wao kama wadau wa maendeleo katika wilaya ya Monduli wakaona wana wajibu mkubwa wa kuungana na Mheshimiwa Rais Dr.John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kupambana na ugonjwa huu mbaya.
Vifaa vilivyotolewa ni Barakoa 350 akikabidhi msaada huo kwa niaba ya viongozi wa Usharika Mchungaji Mathayo Loisulie amesema Kanisa lina wajibu mkubwa katika Kusaidia ustawi wa jamii ikiwemo afya.
Mheshimiwa Iddi Kimanta ameshukuru sana kutolewa kwa misaada hiyo na ameeleza kuwa pamoja na kuwepo kwa ugonjwa ni lazima maisha yaendelee kama kawaida lakini kwa tahadhari zote zinazotolewa na wataalamu wa afya.
