Msichana aliyetekwa nyara Chibok arejea miaka saba baadaye

In Kimataifa

Mmoja wa wasichana wa shule nchini Nigeria waliokamatwa na wanamgambo wa Kiislamu Boko Haram kutoka mji wa Chibok mnamo mwaka 2014 ameachiliwa huru na kujiunga tena na familia yake.

Ruth Ngladar Pogu na mwanaume ambaye anasemekana alimuoa akiwa ameshikiliwa mateka, hivi karibuni walijisalimisha kwa jeshi la Nigeria, kulingana na maafisa.

Wanandoa hao wana watoto wawili.

Zaidi ya wasichana 270 walitekwa nyara huko Chibok, kaskazini mashariki mwa jimbo la Borno.

Zaidi ya wasichana hao 100 wameachiwa huru au wamefanikiwa kutoroka.

Lakini wengine bado hawajulikani walipo.

Ruth Ngladar Pogu na watoto wake walipokelewa na gavana wa jimbo la Borno, maafisa hao walisema.

Walisema sasa atakuwa akiendelea na mpango wa kurekebisha tabia na kuungana tena na jamii ambao utazingatia afya yake na ustawi wa kisaikolojia.

Kati ya mamia ya wasichana waliotekwa nyara kwa mara ya kwanza, wengine walifanikiwa kutoroka muda mfupi baada ya kukamatwa, wakati karibu 100 waliachiliwa huru katika mabadilishano ya wanamgambo wengine wa Boko Haram.

Utekaji nyara umesalia kuwa tatizo kaskazini mwa Nigeria, huku mamia ya wanafunzi wakitekwa mwaka huu pekee.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu