Odinga apinga tarehe mpya ya uchaguzi Kenya.

In Kimataifa, Siasa

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ametangaza kuwa hayuko tayari kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo.

Bwana Odinga amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika, kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo.

Bwana Odinga pia anataka mabadiliko kufanyiwa Tume ya uchaguzi nchini humo, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa wa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa nzuri ambayo ilisababisha kufutiliwa mbali matokeo.

Jana Jumatatu Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya, ilitangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu