Papa Francis akutana na waathirika wa unyanyasaji wa kingono katika mkutano wa vijana katoliki duniani

In Kimataifa

Papa Francis Jumatano alisema kanisa katoliki linahitaji “kujitakasa kwa unyenyekevu na kwa muda mrefu” ili kukabiliana na “kilio cha uchungu” cha waathirika wa unyanyasaji wa kingono waliotendewa na makasisi.

Alikutana na waathirika hao kwa faragha jana Jumatano katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Ureno.

Francis alikuwa akizungumza mjini Lisbon mwanzoni mwa ziara ya siku tano nchini humo ambayo anatumai itawahamasisha vijana wa kikatoliki wakati wa siku ya vijana duniani, tamasha kubwa zaidi la kikatoliki duniani.

Miezi sita iliyopita, ripoti ya tume ya Ureno ilisema takriban watoto 4,815 walinyanyaswa kingono na makasisi kwa zaidi ya miongo saba.

Mzozo huu “unatuomba kujitakasa kwa unyenyekevu kwa muda mrefu, tukianza na kilio cha uchungu cha waathirika, ambao lazima wakubaliwe na wasikilizwe kila mara,” Francis alisema katika hotuba yake kwa maaskofu, mapadre na watawa katika ibada ya jioni ndani ya makazi ya watawa.

Francis alikutana kwa faragha na waathirika 13 walionyanyaswa kingono katika ubalozi wa Vatican mjini Lisbon jana Jumatano jioni, huku Vatican ikisema katika taarifa kwamba mkutano huo ulifanyika katika “mazingira ya usikilizaji mkubwa” na ulidumu kwa zaidi ya saa moja.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA SOMANGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi ya leo  Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua Miundombinu ya barabara kuu

Read More...

HATUTAWAACHIA CCM NAFASI TUTASHIRIKI UCHAGUZI MKUU – ACT WAZALENDO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka

Read More...

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamohanga Afariki Dunia 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu