Polisi yataka Netanyahu ashitakiwa kwa madai ya ufisadi.

In Kimataifa

Polisi wa Israel wamesema wamapata ushahidi wa kutosha wa mashitaka ya rushwa na udanganyifu wa fedha kufunguliwa dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na mke wake Sarah katika kesi ya tatu ya ufisadi inayomkabili kiongozi huyo wa Israel. Inadaiwa kwamba Netanyahu na kampuni ya Bezeq telecom walifanya makubaliano yanye thamani ya mamilioni ya dola ili shirika la habari la Walla ambalo ni kampuni ndogo ya Bezeq liwe linachukua mtazamo chanya wakati linaporipoti taarifa zinazomhusu Netanyahu. Netanyahu amekanusha madai dhidi yake. Uamuzi wa mwisho wa iwapo Netanyahu atafunguliwa mashitaka au la utachukuliwa na mwanasheria mkuu wa Israel ambaye bado anatafakari iwapo amshitaki kuiongozi huyo na kesi nyingine mbili zinazomkabili za madai ya hapo awali ya rushwa, udanganyifu na uvunjaji wa uaminifu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu