Viongozi wa Dini nchini leo wamekutana mkoani Mbeya,katika
Kongamano la kuliombea Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika Kongamano hilo baadhi ya viongozi walipata nafasi ya
kutoa mada na miongoni mwao ni Mwnyekiti wa Jukwaa la
Maridhiano mkoa wa Mbeya Askofu John Oska aliyewasilisha
mada ya Faida ya kushikamana na viongozi katika kuitangaza
nchi ndani na nje ya Nchi.
Katika hatua nyingine viongozi hao wakiendelea na kongamano,
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,aliwapigia simu na
kuwasalimu akiwapongeza kwa jambo hilo zuri wanalolifanya
kwa taifa.



