Rais Magufuli Mbuzi Kukutwa na Virusi.

In Kitaifa

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kushangazwa kufuatia sampuli za Papai, Mbuzi kukutwa na Virusi vya Corona baada ya kupimwa kwenye Maabara kuu ya Taifa.

Rais Magufuli ameyasema hayo hii leo katika hafla fupi ya kumwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Augustine Mahiga aliyefariki dunia.

“Tulipeleka Sample ya Ndege Kware ilikuwa Positive, Mbuzi akawa Positive, Kondoo akawa Negative, ukishaona sampo ukamwambia huyu ni binadamu halafu ana Corona maana yake Mapapai yote yangewekwa Isolation.

“Tulipopeleka sampo ya Papai tukaipa jina la Elizabeth (26) Papai lile lilikuwa Positive kwamba lina Corona, maana yake maji ya Papai ni Positive.

”Tulichukua sampo za Mbuzi, Kondoo, Papai, Oil ya gari tukavipeleka maabara na tukazipa majina, mfano Oil tuliipa jina la Jabir Hamza (30), ili leta Negative, sampo ya Fenesi tuliipa jina la Sarah Samweli (45), matokeo inconclusive.

“Kama tunapeleka sampuli za wanyama zinakutwa Positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, kama mapapai, mbuzi yana corona WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima kuna Watu wameambiwa wana corona wakati hawana

“Mbuzi awe na corona, fenesi liwe na corona, ndege kware awe na corona, lazima tujiulize inawezekana kuna kitu fulani hakijaeleweka Tanzani na hata Duniani hakijaeleweka, natoa wito Wanasayansi Nchi nyingine wachukue sampuli za wanyama, ukuta na yoyote wataamini nachosema

“Tusitishane, kama sampuli maabara inasema papai na fenensi yana corona, inawezekana papai lingekuwa na masikio lingeoza kwa uoga, Waziri Nchemba kachunguze, inawezekana hivi vifaa vimetengenezwa kwamba vikipima Watu 30 anayefuata ana corona, tuwe makini hata na hivi vifaa” amesema Rais Magufuli

Aidha Rais Magufuli ameendelea kuwasisitiza watu wasitishane kisa Corona na badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya ujenzi wa Taifa. 

“Watanzania corona isitutishe, inawezekana kuna Watu wengine wamekufa kwasababu ya hofu tu, Viongozi wa Dini msitupotoshe, nampongeza Mufti amesema sisi tutaendelea kufunga, Watanzania tusimame imara tumeshashinda hii vita.

“Wengine wako Dar es Salaam  wanasema Watu wasiende Bungeni, na nimeagiza wasilipwe posho maana utalipwa kwa kazi uliyofanya, kuna mambo ya ajabu yanafanyika, sina imani na Mkuu wa Mabaara ya Taifa maana haiwezekani tupeleke sampuli za papai zioneshe zina corona.

“Wengine wanazungumza eti tufunge biashara au shughuli za kiuchumi wakati wengine wanaendesha magari yameandikwa STK na inawekwa mafuta na Serikali amesahau alichokalia ndicho kinatoa mafuta, mishahara tutalipaje tukifunga

“Mambo ya kucopy na kupaste Nchi hii hatuwezi kuyafanya, wapo wenzetu waliofunga mipaka na shughuli za kiuchumi mnaona wanavyoteseka, sisi mpaka sasa tuna vifo vya corona 16, huu ni wakati wa kuwapima Watu imani hata Viongozi wa Dini, unawazuiaje Watu kwenda kuabudu

“Mkuu wa Mkoa wa Mtwara nikamuona siku moja anazungumza kwamba Mkuu huyu wa Wilaya amefariki hatuwezi kusafirisha atazikwa hapahapa, ilinisikitisha sana, walishindwaje Viongozi wa Mtwara kumsafirisha DC akaenda kuzikwa kwa heshima kule kwao Moshi!?

“Jaji Mkuu Augustino Ramadhan hapa Mzee wangu alikuwa na tatizo la Kansa tumehangaika nae lakini amefariki Vijana wanapost eti corona…siku hizi hata Mtu akijiua wanasema corona, ikitokea ajali Polisi wamefika kuchukua miili napo corona

“Kwahiyo natoa wito kwa Watanzania tusiogope, tuchape kazi, Wanasiasa waache kutumia corona kuleta manenomaneno, wanasema nifunge Dar es Salaam , sifungi nishasema, nafikiria kuruhusu hata Ligi ya mpira iendelee,tuache kutishana”- Amesema

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu