Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan,leo amepokea Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali
kwa mwaka 2020/2021 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu
wa Hesabu za Serikali CAG pamoja na Ripoti ya TAKUKURU
Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Akiwasilisha ripoti yake kwa Rais Samia Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU ACP Salum Hamduni, ameelezea mambo kadhaa
yaliyofanywa katika kipindi cha mwaka mmoja 2020/21,katika
kudhibiti matumizi ya fedha za umma,ikiwemo na kutoa elimu
dhidi ya vitendo vya Rushwa.
Kwa upande wake Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali CAG amesema Taasisi 19 za umma kati ya taasisi 999
zilizofanyiwa ukaguzi katika mwaka wa fedha 2020/2021
zimepata hati zenye mashaka.
Amesema katika mwaka 2020/21 amefanya kaguzi maalumu 56,
kaguzi 37 zikiwa za mamlaka za Serikali za Mitaa, 12 Serikali
kuu na sita mashirika ya umma na moja ya mifumo ya Tehama.
Mtaa wa mastory kwa uzuri tmeinasa sauti yake alipokuwa
akiwasuilisha ripotihiyo na kuongeza kuwa hati mbaya na
mashaka zimepungua katika ukaguzi huo ikilinganishwa na
mwaka jana.
Huku kukiwa na ongezeko la hati safi kutoka asilimia 89 kwa
mwaka jana hadi asilimia 98.01 mwaka 2020/2021.
Akizungumza baada ya kuzipokea ripot hizo Rais wa Jamuhuri
ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,akiizungumzia
ripoti ya TAKUKURU mbali ya mambo mengine,ameipongeza
Taasisi hiyo kwa kazi nzuri na watanzania kwa ujumla katika
kuwezesha kiwango cha Rushwa kupungua nchini.
Kwa upande wa Ripoti ya CAG Rais Samia ameelezea kwa
ufupi baadhi ya mambo aliyoweza kuyapitia katika ripoti hiyo
likiwemo swala la baadhi ya ndege zikabidhiwe kwa shirika la
ndege ATCL ili vitabu vyao vya mali viae vizuri na kutoa
maagizo kwa wasimamizi wanaohusika kulifanyia kazi hilo.
Insert 04-Samia
Katika hatua yingine Rais Samia akajibu hoja ya wauza dawa
zakulevya kuachiwa na kuagiza swala hilo kufuatiliwa,kwani
watoto wanaharibika.



