RAIS SAMIA ATIMIZA AHADI YAKE KWA KUKAMILISHA DARAJA LA JP MAGUFULI

In Kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametimiza moja ya ahadi zake muhimu kwa Watanzania kwa kuzindua rasmi Daraja la JP Magufuli, linalounganisha miji ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza, mradi mkubwa ulioigharimu serikali Shilingi bilioni 718 kutoka vyanzo vya ndani.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika kushuhudia uzinduzi huo wa kihistoria, Rais Samia alieleza kuwa mradi huo ni sehemu ya maono ya mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ambaye alilenga kupunguza changamoto za usafiri kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

“Kukamilika kwa daraja hili ni hatua kubwa ya maendeleo. Sasa wananchi wanatumia dakika nne kuvuka kutoka Kigongo hadi Busisi, tofauti na awali ambapo walilazimika kutumia muda mrefu na gharama kubwa kuzunguka au kusubiri usafiri wa majini,” alisema Rais Samia.

Akiweka bayana umuhimu wa daraja hilo, Rais Samia alisema kuwa ni alama ya mafanikio ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kwa kutumia rasilimali za ndani. Alisisitiza kuwa daraja hilo si tu linaboresha maisha ya wananchi wa Kanda ya Ziwa, bali pia linachochea ukuaji wa uchumi wa kitaifa na wa kikanda, hususan kwa nchi jirani zilizopo katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Aidha, Rais Samia alieleza kuwa daraja hilo limeondoa hatari zilizokuwepo awali ambapo wananchi walitegemea usafiri wa maji usio salama, hali iliyosababisha ajali na kupoteza maisha pamoja na mali zao. Aliongeza kuwa sasa wananchi watasafirisha bidhaa zao kwa urahisi na gharama nafuu, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ustawi wa shughuli za kiuchumi.

Akigusia historia ya uanzishaji wa wazo la daraja hilo, Rais Samia alieleza kuwa Hayati Dkt. Magufuli aliguswa na tukio la kusikitisha wakati wa safari ya kutoa posa ambapo alilazimika kuzunguka kwa baiskeli baada ya kukuta kivuko hakikuwa salama. Baadaye alielezwa kuwa chombo alichopaswa kutumia kilizama na abiria wote kupoteza maisha.

“Pamoja na kelele na hofu nyingi kutoka kwa baadhi ya watu waliotaka kunikatisha tamaa, niliamua kusimama imara kuhakikisha kuwa ndoto hii ya Hayati Magufuli inatimia. Nilitaka Watanzania waone na kufaidi matunda ya kodi zao,” alisisitiza Rais Samia.

Kwa kukamilika kwa Daraja la JP Magufuli, Tanzania imethibitisha uwezo wake wa kupanga na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati bila kutegemea msaada wa nje, na hivyo kujiimarisha kama taifa lenye uwezo wa kusimamia maendeleo yake kwa ufanisi na weledi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu