Ramaphosa aonyesha matumaini kati ya Ethiopia na TPLF

In Kimataifa

Rais wa Afrika Kusini amesema ana matumaini ya tija katika mazungumzo ya kwanza rasmi ya amani yenye lengo la kumaliza vita vya miaka miwili, kati ya jeshi la Ethiopia na vikosi vya eneo la kaskazini mwa nchi hiyo la Tigray, yaliyoanza nchini Afrika Kusini Jumanne.

Mazungumzo hayo yananuiwa kumaliza mgogoro ambao umepelekea vifo vya maelfu ya watu, mamilioni kuyahama makazi yao na kuwaacha maelfu katika hali mbaya ya njaa katika taifa hilo la pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, hali inayoelezwa kuyumbisha eneo zima la Pembe ya Afrika.

Mazungumzo hayo yatakamilika Jumapili, serikali ya Afrika Kusini ilisema.

Afrika Kusini “inatumai mazungumzo yataendelea kwa njia yenye tija na kuleta mafanikio ambayo yatasababisha amani ya kudumu kwa watu wote wa nchi dada yetu mpendwa Ethiopia,” alisema Vincent Magwenya, msemaji wa Rais Cyril Ramaphosa.

Timu ya upatanishi ya Umoja wa Afrika inaongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, akisaidiwa na rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu rais wa zamani wa Afrika Kusini, Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa Marekani walishiriki kama waangalizi, Umoja wa Afrika ulisema.

Mazungumzo hayo, yanayoongozwa na Umoja wa Afrika, yanaanza wakati serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imedai kupata mafanikio makubwa katika vita hivyo na kuiteka miji kadhaa mikubwa ya Tigray katika wiki iliyopita.

Mashambulizi hayo ya serikali yaliyofanywa kwa pamoja na wanajeshi washirika kutoka nchi jirani ya Eritrea, yameibua hofu ya madhara zaidi kwa raia, na kusababisha viongozi wa Afrika, Marekani na Ulaya na hata Papa Francis kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano na mazungumzo ya haraka.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu