–
Kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index(GPI) inayotolewa na Taasisi ya Uchumi na Amani, Tanzania imeshika nafasi ya 7 kwa kuwa nchi yenye amani kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara
–
Kidunia, Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 51 mwaka 2018 hadi nafasi ya 54 mwaka 2019 kati ya nchi 163 huku Iceland, New Zealand, Uholanzi, Austria, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, na Czech zikiorodheshwa kuwa na amani zaidi Duniani
–
Wakati Tanzania ikiongoza Afrika Mashariki, Rwanda imeifuata ikiwa ya pili Afrika Mashariki lakini imeshika nafasi ya 17 kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikifuatiwa na Uganda iliyoshika nafasi ya 23 na kisha Kenya ambayo ni ya 28
–
Nchi zilizoshika nafasi za juu katika eneo la jangwa la Sahara ni Mauritius, Botswana, Malawi, Ghana, Zambia na Sierre Leone huku Burundi, Chad, Cameroon, Mali, Nigeria, DR Congo, Somalia na Sudani Kusini zikishika nafasi za chini