SERIKALI inakusudia kufuta vyama vya ushirika 3436 nchi nzima kutokana na kukiuka kifungu cha 100 cha Sheria ya kuanzisha vyama hivyo.
Serikali imefikia hatua hiyo, baada ya kubainika kuwa vyama hivyo vinakwenda kinyume na taratibu ya kuanzisha kwake,ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwasilisha taarifa ya mwaka.
Akizungumza katika mji wa kiserikali Mtumba mkoani Dodoma Waziri wa Wizara ya kilimo Mh.Japhet Hasunga amewaambia waandishi wa habari kuwa wanakusudia kuvifuta vyama hivyo kwa kukiuka Mashariti ya kuanzishwa kwake.
Kabla ya kusudio la kuvifuta vyama hivyo, Waziri amemuagiza Mrajisi wa vyama hivyo kutangaza kusudio hilo katika gazeti la serikali ambapo vyama vitakavyokuwa na malalamiko vitasikilizwa ndani ya siku hizo tisini.
Ameongeza kuwa vyama vingi ni matokeo ya mfumo wa uwezeshaji wananchi kiuchumi ujulikanao kama (JK found) uliolenga kuwanyanyua kiuchumi.
Awali kabla ya tangazo la kuvifuta vyama hivyo,kulikuwa na jumla ya vyama elfu 11na 149 ambapo sasa takriban vyama Elfu 7 Mia 7 na 10 ndivyo vitasalia vikiwa hai.



