Serikali kupitia kwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
imepanga kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 5.5 kwa mwaka wa
Fedha 2022/23 kwa ajili ya kuendeleza ubunifu nchini.
Hayo yameelezwa na katibu mkuu wizara hiyo Prof Eliaman
Sedoyeka,wakati akizungumza na wanahabari kwenye mafunzo
ya wiki ya ubunifu kwa mwaka 2022,inayotarajiwa kuanza
Tareher 15 mwezi huu hadi Tarehe 20 jijini Dodoma.



