SERIKALI YAPOKEA MSAADA KUKABILIANA NA CORONA (COVID-19).

In Kitaifa

Ubalozi wa China nchini Tanzania umeipatia Serikali msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kuendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 (Corona), na kuahidi kuendelea kushirikian na Serikali ya Tanzania kukabiliana na ugonjwa huo, hadi hapo utakapomalizika.

Akipokea vifaa hivyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema msaada huo utaenda kwa watumishi wa afya kote nchini kwani serikali imetoa kipaumbele cha kwanza kwao ili kuweza kuwakinga na maambukizi ya Covid-19.

“kwa niaba ya serikali tunaishukuru sana Serikali ya China kwa mchango huu, na niendelee kuwathibitishia wale wote mnaoisaidia Serikali ya Tanzania,msaada huu tutaupeleka kwa watumishi wa afya,kipaumbele ni kuwakinga watumishi wa afya wasipate maambukizi”

Kwa upande wake balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke amesema nchi yake na Tanzania ni marafiki kwa muda mrefu na ugonjwa huo ulipoikumba Nchi yao kwa mara ya kwanza, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono katika mapamabana dhidi ya ugonjwa huo, hivyo na wenyewe wamejitoa kuisaidia kukabiliana nao.

Mhe.Wang Ke amesema Serikali ya China kwa sasa imechukua hatua na kujitoa rasmi kuwa nchi itakayoisaidia Tanzania katika misaada ya dharura ya vifaa kinga ambayo itasaidia kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Mwisho.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu