SERIKALI Imetoa Wito kwenye mifuko yote ya uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kuhakikisha wanapitia upya viwango vya Riba katika mikopo ambayo wamekuwa wakiitoka wa wananchi kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini.
Wito huo umetolewa na waziri wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania KASIMU MAJALIWA kwenye uzinduzi wa wa maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi ambayo yanafanyika mjini Dodoma.
Waziri MAJALIWA amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiogopa kukopa katika mifuko hiyo kutokana na kuwa na liba kubwa ingawa wanapenda kukopa ili waweze kujikomboa kiuchumi pia ameeleza kutokana na liba hiyo wanaona watashindwa kurejesha mkopo na mwisho wake watauziwa nyumba zao .
Hata hivyo amesema kuwa kila mfuko wa uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi ianze kujitangaza pamoja na kujipambanua katika kazi zake ambazo wanazifanya na kwa ile mifuko ambayo bado awajafikia hatua hiyo na wao waanze kujipambanua kama mifuko mingine.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza uwezeshaji kwa wananchi kiuchumi Taifa JOHN JINGU amesema kuwa watahakikisha kila mfuko hiyo inakuwa na kiwanda katika sehemu zao ambazo wanafanyia kazi pia amesema kwa kufanya hivyo wataweza kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana hapa Nchini.
