Serikali imeeleza kuwa fedha za mfuko wa majimbo zipo kwa
ajili ya kuchochea maendeleo ya wananchi na sio za kununulia
thamani za ofisi za wabunge.
Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tamisemi David Silinde,ambaye amesema kuwa
fedha hizo za mfuko zipo mahususi kwa ajili ya kuchochea
maendeleo kwa wananchi.
Silinde alikuwa anajibu swali la Mbunge wa Lulindi CCM Issa
Mchungahela,ambaye ameuliza ikiwa Fedha za Mfuko wa
Jimbo zinaweza kutumika kununulia thamani za ofisi ya jimbo.



