Polisi katika mkoa wa Tabora inawashikilia watu 3 kwa tuhuma
za kuhusika na mauwaji ya diwani wa kata ya usunga wami
wilaya ya sikonge bwana Alfred Lucas Masamalo.
Mbali na watu hao pia naibu kamanda wa polisi mkoani humo
ACP Laurian Fabian ametangaza kukamatwa kwa watu sita
waliohusika kumuua askari wa jeshi la Tanzania.
ACP Laurian Fabian ameeleza hayo alipokuwa akitoa taarifa
yake kwa wanahabri juu ya matukio mbali mbali ya kihalifu
waliyofanikiwa kuyadhibiti mkoani humo.



