Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mohamed Mchengerwa, ameitaka
Takukuru kufuatilia matumizi ya fedha zaidi ya Bilioni 396
zilizopelekwa katika majimbo yote nchini,kwa ajili ya ujenzi wa
barabara kwa kiwango cha lami.
Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo kwenye uzinduzi
wa kituo cha kumbukumbu za nyaraka za Umma Kanda ya Ziwa
kilichopo mtaa wa Lumala Mashariki wilayani Ilemela mkoani
Mwanza.
Katika maelezo yake amesema kuwa serikali imetoa Bil 1.5 kwa
kila jimbo nchini kwa ajili ya ujenzi huo.



