Uhusiano wa Young Thug na Elton John unaendelea kushamiri, haswa baada ya kuwa pamoja katika kuandaa ngoma iitwayo “High”.
Wakati wa mahojiano ya hivi karibuni na Billboard, icon wa mziki aina ya English rock alikiri kushangazwa na uwezo wa freestyle ya Thugger wakiwa studio kuliko uwezo wa Eminem aliokuwa amemwonyesha.
“Namaanisha, nimeona Marshall [Mathers] akifanya hivyo katika Detroit, lakini sijawahi kuona mtu kama Thug akiingia na kufanya hivyo.
“High” ilitolewa mnamo 2018, lakini wawili hao walikutana miaka kabla wimbo huo haujatoka. Katika mazungumzo yao, Elton John alimhimiza Young Thug kuimba zaidi katika muziki wake.



