Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI,leo imetoa tuzo za ubora wa Taaluma kwa shule za msingi na sekondari kwa mwaka 2022 kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri mwka 2021.
Tuzo hizo zimetolewa jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo manaibu waziri na Mgeni Rasmi alikuwa waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa.
Kabla ya mgeni Rasmi kuzungumza alitanguliwa na Katibu mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI Professor Riziki Shemdoe ambaye alitoa utangulizi juu ya tuzo hizo.
Kwa upande wake Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Innocent Bashungwa,mabli na upongeza waandalizi wa tukio hilo,amezungumza mambo kadhaa katika likiwemo la jitihada za serikali katika kuhakikisha inaboresha mazingira ya elimu nchini.



