Serikali imesema ipo tayari kutumia dawa mpya ya saratani ya
utumbo iliyo gunduliwa huko nchini Marekani,endapo shirika la
Afya ulimwenguni litaipitisha na kuridhia matumizi ya dawa
hizo.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugezi wa Taasisi ya utafiti wa
magonjwa ya binadamu hapa nchini NIMRI Prof Yunus Mgaya,
wakati wa kongamano la maswala ya utafiti ambayo imefanyika
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Amesema wao kama kituo cha utafiti watakuwa tayari kuifanyia
Majaribio ya kuridhia,endapo kama dawa hiyo itapitishwa na
WHO pamoja na kukidhi vigezo vya mamlaka ya vyakula na
dawa nchini TMDA.
Mtaa wamastori kwa uzuri tumeinasa sauti ya mkurugezi wa
Taasisi hiyo Prof Yunus Mgaya akibainisha hayo.
