Tekashi akataliwa msaada alioutoa kwa No kid hungry foundation.

In Kimataifa

Msanii tekashi 69 ameendelea kushika vichwa vya habari, na leo amekuja na
jipya hii ni baada ya tekashi kukataliwa msaada aliokuwa ameutoa kwa no kid
hungry foundation.


Jana msanii Tekashi 69 ambae ameweza kuvunja rekodi na ngoma yake mpya
ya Gooba akiwa na view millioni 126 ndani ya siku nne tu. Jana Tekashi 69
kupitia kurasa wake wa Instagram alipost na kuandika kwamba atatoa dolla za
kimarekani laki mbili, ambayo ni sawa sawa na tsh.440,000,000, ambayo
alisema kwamba anaitoa kwa ajili ya shirika la no kid hungry foundation,
linalojishughulisha na kuhakikisha watoto hasahasa wa mitaani wanapata
chakula. Lakini haikuenda kama alivyotarajia na hii ni baada ya shirika hilo
kukataa mchango wake huo na kusema kwa kupitia msemaji wa shirika hilo,
Laura Washburn, kwamba wanashukuru kwa mchango wa Mr.Fenandes
(Tekashi 69) lakini hawatauchukua, sababu kuu ikiwa ni kwamba pamoja na

kuwa wanahitaji michango mingi, hawawezi kuchukua michango kutoka kwa
mtu ambae maadili yake yanapingana na maadili ya shirika lao hilo.
Na Tekashi 69 hakufurahishwa na hili, kwani alirudi Instagram na kusema kwa
kulalamika kwa hio bora watoto wakae njaa kuliko mchukue pesa kutoka
kwangu. Lakini baby mama wake akarudi tena kwenye Instagram story yake na
kusema kwamba Tekashi ni mnafiki, anajidai kutoa pesa kwa watoto wakati
hatoi matunzo ya mtoto wake mwenyewe, na kusema kwamba anajuta ni
kwanini aliandika barua kwa hakimu kumuombea awez kutoka kwa ahadi ya
kuwa angemsaidia na kumpa matumizi ya mtoto lakini tangu ametoka hajafanya
chochote.


Lakini pia baada ya kujigamba na kutaka aitwe king of New York baada ya
kuvunja rekodi na wimbo wake huu mpya, wasanii malegendary pia wamekuja
na kumjibu ambapo kwa mara nyingine tena Meek Mill alipost akasema
anashangaa kwanini watu wanashabikia ujinga wa snitch, na watu wanasahau
kwamba aliyemuua Nipsyey Hussle alikua ni snitch vilevile, lakini pia Snoop
dog aliandika kupitia twitter yake kwamba mtu yoyte anaesntich yeye
hamkubali, na kama unamkubali mtu ambae ni snitch wewe pia unakuwa
umefeli, lakini wasanii wengine kama Gucci manne, Drake na Young Thug pia
wameonyeshwa kutokumfagilia wala kumkubali Tekashi kwa sababu ya
kuwasnich wenzake.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

MAJALIWA ATOA RAI KWA WAMILIKI WA MALORI KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa malori nchini wawajali madereva na wahudumu wa magari hayo ikiwa ni pamoja

Read More...

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu