Tetesi za Soka Ulaya

In Kimataifa, Michezo

Paris St-Germain wanataka dau la £188m kutoka Real Madrid kwa ajili ya mshambuliaji wake Mfaransa Kylian Mbappe, 22. (Le Parisien – in French)

Manchester City wanaweza kumgeukia mshambuliaji wa Juventus na Ureno Ronaldo, 36, baada ya nahodha wa England, Harry Kane kusema anabaki Tottenham. (ESPN)

Kane, 28 amesikitishwa na mwenyekiti wa Tottenham chairman Daniel Levy kutoruhusu aondoke na naweza akasaini mkataba mpya. (Telegraph)

Harry Kane

Meneja Pep Guardiola ataondoka Manchester City pale mkataba wake utakapomalizika msimu wa mwaka 2022-23 ili kupumzika kabla ya kuhamia kufundisha timu za taifa. (Globo, via Manchester Evening News)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta hayuko katika hatari ya kutimuliwa kibarua chake licha ya washika bunduki hao kuanza vibaya msimu hiu wa ligi kuu ya England.

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anahusishwa na mipango ya kuchukua nafasi ya Arteta. (Independent)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta hayuko katika hatari ya kutimuliwa kibarua chake
Maelezo ya picha,Meneja wa Arsenal Mikel Arteta hayuko katika hatari ya kutimuliwa kibarua chake

Meneja wa Roma Jose Mourinho amepanga kutumia £13.5m kwa ajili ya kiungo wa Chelsea muingereza Ruben Loftus-Cheek, 25. Nyota huyo aliwahi kidogo kufanya kazi na Mourinho wakati mreno huyo aliporejea kuifundisha Chelsea kwa mara ya pili. (Mail)

Manchester United haitaweza kupeleka dau kwa ajili ya kiungo wa Rennes mfaransa Eduardo Camavinga, 18, au kiungo wa Atletico Madrid na Hispania Saul Niguez, 26, kama haitauza wachezaji wake kupata fedha za kuingia sokoni. (ESPN)

Chelsea wanaelezwa wako katika nafasi nzuri ya kumsajili Niguez, huku Atletico wakiwa tayari kumuuza Mhispania huyo. (Express)

Saul Niguez

Sevilla wanasema walikataa ofa ya Chelsea kwa ajili ya mlinzi wake mfaransa Jules Kounde,22 na hawahitaji kuuza wachezaji. (Goal)

Kiungo wa Barcelona Ilaix Moriba huenda akatua Chersea ama RB Leipzig kama kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 raia wa Guinea hataongeza mkataba mpya na wakali hao wa Laliga. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Winga wa Arsenal na Brazil Willian, 33, anajaribu kukamilisha uhamisho wake kuelekea Corinthians. (Sun)

Willian
Maelezo ya picha,Winga wa Arsenal na Brazil Willian, 33, anajaribu kukamilisha uhamisho wake kuelekea Corinthians

Koungo wa zamani wa Arsenal na England Jack Wilshere, 29, anafikiria kustaafu soka baada ya kukosa ofa ya kujiunga na klabu yeyeote tangu aachwe na klabu ya Bournemouth. (Athletic)

Kiungo wa Barcelona na Hispania Sergio Busquets amekubali kukatwa tena mshahara wake ili kusaidia wakali hao wa Laliga kupunguza mzigo wa mishahara klabuni. (ESPN)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu