Uchunguzi CORONA Wasimama

In Uncategorized

Juhudi za kuchunguza vyanzo au chimbuko la virusi vya corona ambavyo hadi sasa vimesababisha vifo vya mamilioni ya watu na kulemaza chumi za mataifa ulimwenguni, zimesimama, huku muda ukizidi kuyoyoma. Hayo yamesemwa jana Jumatano na wanasayansi waliotwikwa jukumu na Umoja wa Mataifa la kuchunguza chanzo cha virusi hivyo. Katika taarifa yao, wamesema kadri muda unavyosonga, ndivyo uchunguzi wa chimbuko la virusi hivyo vilivyoripotiwa mwanzo Wuhan nchini China mwishoni mwa mwaka 2019 unazidi kuwa mgumu huku ushahidi ukitoweka au kuharibiwa. Taarifa hiyo imejiri chini ya wiki mbili tangu Shirika la Afya Duniani WHO lilipoihimiza China kutoa habari kuhusu visa vya mwanzo vya corona. Ripoti ya awali iliyotolewa na wataalam wa kimataifa waliotumwa nchini China na WHO mwezi Januari, kuchunguza chimbuko la virusi hivyo, ilisema kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba virusi hivyo vilitoka kwa popo hadi kwa wanadamu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu