Real Madrid wanapanga mikakati itakayomuwezesha
mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30,
kuondoka kwa uhamisho bila malipo. (Marca)
Manchester City wametanga £80m kuwa bei ya kumuuza winga
wa Algeria Riyad Mahrez, 29, ambaye amehusishwa na
uhamisho wa kuenda Paris St-Germain. (Sun)
Manchester United wanapanga ‘mkakati’ wa kusaini mkataba na
beki wa Barcelona na Ufaransa Samuel Umtiti, 26 msimu huu.
(Talksport)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anataka kumuuza kiungo wa
kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 31, msimu wa joto huku
wakiwa na mpango wa kubadili mkataba ake wa mkopo kuwa
uhamisho wa kudumu . (Express)