Tetesi za Soka Ulaya leo Jumatatu Septemba 20, 2021

In Kimataifa, Michezo

Barcelona wanajiandaa kuwasilisha ofa za kuwanunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, nyota wa Ufaransa na man united Paul Pogba, 28, na mchezaji wa Uhispania Dani Olmo, 23. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Huku mkataba wa Pogba wa Manchester United ukikamilika majira yajayo ya joto , kilabu hiyo imejiandaa kutoa ofa ya Pauni 400,000 kwa wiki kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara wa juu zaidi katika Ligi Kuu ya England wakati wote. (Express)

Kiungo Jesse Lingard, 28, na beki Eric Bailly, 27, ni miongoni mwa wachezaji saba ambao wanaweza kuuzwa na Manchester United mwezi Januari. (Sun)

Chelsea itakabiliana ana kwa ana na Juventus kupata saini ya kiungo wa chini ya umri wa miaka 21 wa Ufaransa na Monaco Aurelien Tchouameni, 21, mnamo Januari. (Tuttomercatoweb – in Italian)

Liverpool, Tottenham na Juventus wamepania kupigania winga wa Bayern Munich na Ufaransa Kingsley Coman, 25. (Fichajes – in Spanish)

Chelsea pia inavutiwa na Coman baada ya mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Bayern Munich kumtaka aondoke klabuni. (Mirror)

Bosi wa Barcelona Ronald Koeman hajui hatma yake iko vipi wakati kukiwa na ripoti kwamba rais Joan Laporta anaunda orodha ya watu wanaochukua usukani wa kilabu hiyo (Express)

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 28, anaweza kuwa bado anahisi athari za uhamisho wake ulioshindwa kufanyika wa Manchester City msimu huu wa joto. (TalkSport)

Juventus walikuwa wamepanga kumsaini Gianluigi Donnarumma, 22, bila malipo kutoka AC Milan msimu huu wa joto, lakini walilazimika kujiondoa kwa sababu za kifedha, na kuiruhusu Paris St-Germain kumchukua (Goal)

Mkurugenzi wa michezo wa PSG Leonardo amepuuza maoni kwamba nyota wa Argentina Lionel Messi, 34, atapata zaidi ya pauni milioni 30 kwa msimu wakati wa mkataba wake wa miaka mitatu. (Mail)

tl

Manchester United inawasiliana na kiungo wa England Jesse Lingard, 28, juu ya mkataba mpya. Bruno Fernandes na Luke Shaw pia wako kwenye ‘orodha ya wanaozingatiwa kwa mkataba’ na kilabu hiyo . (Fabrizio Romano)

Arsenal inaandaa dau la pauni milioni 20 kwa Winga wa Uholanzi mwenye chini ya umri wa miaka 21 na winga wa Club Bruges Noa Lang, 22. (Fichajes via Mirror)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu