Trump kusimamisha mchango wa Marekani kwa (WHO)

In Kimataifa

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema, kwa muda
mfupi atasimamisha mchango wa Marekani kwa Shirika
la Afya Duniani (WHO) huku ikifanywa tathmini ya jinsi
shirika hilo lilivyoshughulikia mripuko wa virusi vya
corona mara tu baada ya kuzuka.


Trump analishutumu shirika hilo la afya la Umoja wa
Mataifa kwa jinsi lilivyoshindwa kushughulikia kuenea
kwa ugonjwa wa COVID-19.

Trump amedai katika mkutano na waandishi habari katika
ikulu ya White House kwamba iwapo shirika la WHO
lingefanya kazi yake vizuri na kutuma wataalamu wa afya
China, basi mripuko huo ungeweza kudhibitiwa.


Ameongeza kwamba shirika la WHO limeshindwa
kutimiza jukumu lake la msingi na lazima liwajibishwe.
Trump pia amesema shirika la WHO limeiunga mkono
China kwa kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu virusi vya
corona.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu