Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itafanya Uchaguzi mdogo kwenye Jimbo la Buyungu, Mkoani Kigoma na kwenye Kata 79 za Tanzania Bara, Mwenyekitiwa NEC, Jaji (R), Semistocles Kaijage amesema.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Jaji Kaijage amesema Uchaguzi utafanyika tarehe 12 mwenzi ujao (Agosti) na fomu zauteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 8 hadi 14 mwenzihuu (Julai).
“Uteuziwa Wagombea utafanyika tarehe 14 Julai, mwakahuu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 15 Julai, hadi tarehe 11 Agosti, mwaka huu nasiku ya Uchaguzi itakuwani tarehe 12 Agosti mwaka huu,” alisema.
Jaji Kaijage amebainisha kwamba Tumetangaza uwepo wa nafasi za wazi ya Ubunge kwenye Jimbohilo la Buyungu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Ndugu Job Ndugai.
“Tumeipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwakuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi ya wazi ya Mbunge wa Jimbo la Buyungu katika Halmashauri ya Kakonko Mkoani Kigoma kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbohilo Mheshimiwa Kasuku Samson Bilago,” alisema.
Kwa upande wa nafasi za wazi za Udiwani, Mwenyekiti huyo alisema Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana akitaarifu juu ya uwepo wanafasihizo na taratibu za uchaguzi mdogo zikaanza maramoja.
“Tumeipokea Taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi za wazi za Madiwani katika Kata 79 za Tanzania Bara,” alisema.
Akitoa wito kwa vyama vya Siasa, Jaji Kaijage amesema “tunapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wauchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yote wakati wa kipindi cha Uchaguzi mdogo”.
Jaji Kaijage alisema kwamba uchaguzi huo mdogo utafanyi kanda ya Halmashauri 43 zilizopo kwenye Mikoa 24 ya Tanzania Bara.
Mikoa hiyo ni pamoja na Kigoma, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Mbeya, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida, Songwe, Tabora naTanga.
Halmashauri hizo ni pamoja na Moshi, Ruangwa, Mbulu, Hanang, Babati, Serengeti, Tarime, Kyela, Mtwara, Newala, Kilombero, Kilosa, Kwimba, Makete, Wanging’ombe, Kalambo, Songea, Msalala, Meatu, Singida, Songwe, Tunduma, Tabora, Nzega, UrambonaTanga.
Halmashauri nyingine ni pamoja na Karatu, Longido, Arusha, Ngorongoro, Monduli, Meru, Ubungo, Kondoa, Mpwapwa, Chamwino, Iringa, Kyerwa, Misenyi, Muleba, Nsimbo, Kasulu na Same.



