Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya amesema kuwa
baada ya kufanya ziara ya kutembelea vyuo mbali mbali vya
kilimo hapa nchini amegunduakuwa moja ya changamoto
iliyopo ni upatikanaji wa vitabu vya kiada na ziada.
Katibu mkuu huyo ameyaeleza hayo alipokuwa akizungumzia
upatikanaji wa njia ya kisasa ya wanavyuo kusoma vitabu kwa
mfumo wa Kielctronik,ambayo itasaidia kutatua lile tatizo la
ukosefu wa vitabu.



