Viongozi wa Afrika Mashariki wamekubaliana jana Jumatatu
kutuma jeshi la kikanda mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na kutoa mwito wa mapigano
kusitishwa mara moja.
Hatua hiyo ilitangazwa aa ofisi ya rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta baada ya wakuu wa mataifa saba ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki kufanya mazungumzo mjini Nairobi kuhusiana na
kuongezeka kwa machafuko mashariki mwa Kongo.
Kulingana na ofisi hiyo ya rais Uhuru Kenyatta, wakuu hao
wameliagiza jeshi hilo la kikanda kushirikiana na vikosi vya
Kongo kurejesha utulivu na kuhakikisha amani inapatikana.
Hata hivyo taarifa hiyo haikusema iwapo Rwanda inayolaumiwa
kuwasaidia waasi itaunganishwa kwenye jeshi hilo, ingawa
serikali ya Kongo inasisitiza haitakubali wanajeshi hao
kujumuishwa.



