Vurugu zimeibuka katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM
Wilaya ya Dodoma, baada ya baadhi ya Wanachama wa chama
hicho kudai kuwa majina ya Wagombea Udiwani yaliyopitishwa
yamebadilishwa bila sababu za msingi katika baadhi ya kata za
Wilaya ya hiyo.
Katibu wa CCM kata ya Ipagala Minudi Daniel alijikuta katika
wakati mgumu, baada ya kutoka nje ya ofisi hizo kwa lengo la
kuwafafanulia wanachama wake kinachoendelea,na baadaye
Polisi walifika na kutuliza ghasia hizo.
