WAMASAI WAANDAMANA KATIKA UBALOZI WA KENYA

In Kitaifa

KUIOMBA SERIKALI YA KENYA KUINGILIA KATI UPOTOSHAJI WA ZOEZI LINALOENDELEA LA LOLIONDO NA NGORONGORO UNAOFANYWA NA ASASI ZA KIRAIA PAMOJA NA WANAHARAKATI WAISHIO NCHINI HUMO

WAMAASAI KUTOKA MAENEO MBALIMBALI WAMEFANYA MAANDAMANO YA AMANI HADI UBALOZI WA KENYA TANZANIA, ULIOPO OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM LEO JUNI 17, 2022 KUIOMBA SERIKALI YA KENYA IINGILIE KATI UPOTOSHAJI UNAOFANYWA NA ASASI ZA KIRAIA NA WANAHARAKATI KATIKA ZOEZI LA KUHAMA KWA HIARI LINALOENDELEA KATIKA WILAYA YA NGORONGORO PAMOJA NA TARAFA YA LOLIONDO.

WAMASAI HAO WAMEELEZA KUWA UPOTOSHAJI HUO UMELENGA KUICHONGANISHA JAMII YA WAMAASAI NA SERIKALI YA TANZANIA, PAMOJA NA KUZOROTESHA JITIHADA MBALIMBALI ZA MAKUBALIANO ZILIZOFIKIWA NA PANDE ZOTE MBILI.

HAYO YAMEELEZWA KUPITIA BARUA YA PAMOJA ILIYOSAINIWA NA KATIBU WA UMOJA HUO ANAYETAMBULIKA KWA JINA LA LOISHIYE LASHILUNYE ILIYOSOMWA NA KIONGOZI WA MSAFARA ALIYEJITAMBULISHA KWA JINA MOJA LA EMANUEL.

HATUA HII INAKUJA BAADA YA ZOEZI LA KUWEKA ALAMA ZA MIPAKA KATIKA ENEO LA LOLIONDO PAMOJA NA UHAMAJI WA WANANCHI WA NGORONGORO AMBAPO LICHA YA SERIKALI KUTANABAISHA UWEPO WA MAKAZI MAPYA KATIKA ENEO LA HANDENI, KUMETOKEA UPOTOSHAJI NA UCHOCHEZI UNAOLENGA KUKWAMISHA ZOEZI HILO.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu