Mkuu wa wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amewataka
wanaume wilayani humo kuachana na tabia za kusoma SMS za
wake zao.
Kauli hiyo imetolewa leo April 5 2022 na Mkuu huyo wakati wa
ibada ya mazishi ya mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka
35 mkazi wa kijiji cha Kwankonje aliyefariki dunia kwa
kukatwakatwa na mapanga huku chanzo kikidaiwa kuwa ni
wivu wa kimapenzi.



