Kuna taarifa imetolewa na Mbunge wa Mikumi na Mwanamuziki Mkongwe wa Hip-Hop Nchini, Joseph Haule maarufu kama Professor J kwamba usiku wa jana Majira ya Saa moja kuna watu waliovamia Studio za Tongwe Records na kuwateka Wasanii Wawili wa Hip-Hop, Roma Mkatoliki na Moni Central Zone.
Professor Jay ametumia Mtandao wa Instagram kutoa taarifa hizo ambapo amepost picha ya Roma Mkatoliki na Moni na kuandika Maneno haya hapa chini:-
ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..
Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!
Watanzania Wametoa maoni Tofauti Tofauti kupitia Tukio hilo unaweza kuyafuatilia kwenye Post hiyo Live Instagram hapa chini
Bado tunafuatilia undani wa Tukio Hilo endelea kusikiliza Radio5
