Wasanii wa Hip-Hop Tanzania, Roma na Moni Central Zone Wametekwa na Watu wasiojulikana jana

In Burudani

Kuna taarifa imetolewa na Mbunge wa Mikumi na Mwanamuziki Mkongwe wa Hip-Hop Nchini, Joseph Haule maarufu kama Professor J kwamba usiku wa jana Majira ya Saa moja kuna watu waliovamia Studio za Tongwe Records na kuwateka Wasanii Wawili wa Hip-Hop, Roma Mkatoliki na Moni Central Zone.

Professor Jay ametumia Mtandao wa Instagram kutoa taarifa hizo ambapo amepost picha ya Roma Mkatoliki na Moni na kuandika Maneno haya hapa chini:-

ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..
Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!

Watanzania Wametoa maoni Tofauti Tofauti kupitia Tukio hilo unaweza kuyafuatilia kwenye Post hiyo Live Instagram hapa chini


Bado tunafuatilia undani wa Tukio Hilo endelea kusikiliza Radio5

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKAGUA BARABARA YA SOMANGA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi ya leo  Aprili 16, 2025 amewasili eneo la Somanga kukagua Miundombinu ya barabara kuu

Read More...

HATUTAWAACHIA CCM NAFASI TUTASHIRIKI UCHAGUZI MKUU – ACT WAZALENDO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka

Read More...

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Gissima Nyamohanga Afariki Dunia 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu