Watanzania watakiwa kucheki afya zao na kufuata ushauri wa daktari.

In Afya

Watanzania wametakiwa kuwa na mazoea ya kwenda vituo vya afya kucheki afya zao na kuacha dhana ya kutumia dawa bila kufuata ushauri wa daktari
Wito huo umetolewa na Dr,Meshak Athman mkurugenzi wa Yeriko Sanitarium Clinic wakati akizungumzia namna watu wanavyoshindwa kutofautisha magonjwa ambapo amesema ugonjwa unaokuwa ni changamoto ni UTI na KISONONO ambayo ni magonjwa ya zinaa


Amesema kisonono dalili zake ni wakati wa kushiriki tendo la ndoa kwa mwanaume inaonesha dalili kwa haraka hasa kwenye mfumo wa haja ndogo, ndani ta masaa 12 hadi 24 na kupata maumivu makali wakati anapoenda haja ndogo na usaha mzito,
Pia amesema dalili za UTI ni kupata haja ndogo mara kwa mara, kupata maumivu ya tumbo la chini, kutoka uchafu mweupe kwenye haja ndogo 


Dr. Meshak amesema kuwa ni vizuri watu kufanya vipimo ili kuweza kujua ugonjwa unaokusumbua kwani watu wengi wamekuwa wakitumia dawa nyingi sana ambazo hazisaidii kumaliza tatizo na badala yake kuleta madhara makubwa ambayo tanaweza kupelekea hata kupoteza maisha
Pia amewataka watanzania kuchukua taadhari kabla ya kupata madhara kwenye miili yao ikiwa ni pamoja na kuacha ngono zembe, kula vyakula vyenye virutubisho na kufanya mazoezi mara kwa mara

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu