WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

In Afya, Kitaifa

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa inatarajia kutoa chanjo kwa watoto 109, 514 .

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Halmashuri ya Nkasi Dkt.Benjamin Chota ambapo amesema hamasa  na elimu ilishaanza kutolewa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kanisani, misikitini pamoja na vituo mbalimbali vya redio.

“Sisi kama Halmashauri tulianza kutoa hamasa  na elimu katika maeneo mbalimbali na lengo ni kuwafikia watoto 109,514  wenye umri chini ya miaka 8 na sehemu kubwa ambayo tunategemea kuwapata watoto ni maeneo ya shuleni na nyumba kwa nyumba pia “

Aidha,Dkt.Chota ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi la kampeni ya Polio kwani mtoto asipopata chanjo anaweza kupata ulemavu wa kudumu.

“Ni chanjo muhimu kuwakinga watoto wetu na ugonjwa wa kupooza na madhara  makubwa ni ulemavu wa kudumu hivyo, jamii naiomba kutoa ushirikiano pindi timu za uchanjaji zinapopita ikiwezekana tupate watoto wengi zaidi ya lengo”amesema.

Ikumbukwe kuwa Kampeni ya Chanjo ya Matone dhidi ya ugonjwa wa Polio inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 21, Septemba 2023 katika Viwanja vya Ndua  Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa na Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu na itafanyika hadi Septemba 24, 2023 katika mikoa 6 ya Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya huku walengwa ni watoto wote walio chini ya miaka 8.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu