Watu 10 Wajeruhiwa kwa ajali Morogoro

In Kitaifa

Watu 10 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha lori aina ya Scania lenye tela  namba T 394 DHK na Costa ya abiria yenye namba T 147 DHZ,  inayofanya safari za  Mbezi kwenda Morogoro.
 Imeelezwa kuwa kati yao, majeruhi wanne wako mahututi, wamepelekwa hospitali. Akizungumza katika eneo la ajali hiyo, Kamanda wa  Polisi, Willbroad Mutafungwa amesema tela la lori namba T 394 lilikatika katika kiunguo cha kichwa cha lori hilo na kuangukia basi dogo  katika maeneo ya Junior Seminary. Kamanda Mutafungwa amewataka madereva kuwa makini barabarani. Dereva wa lori hilo amekimbia na anatafutwa na polisi. Pia, Kamanda wa Jeshi la   Zimamoto na Uokoaji, Goodluck  Zelothe amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo walifika mara moja wakiwa na vifaa vya uokoaji. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Ole Sanare, amewaonya madereva na wamiliku wa magari kufanya ukaguzi wa magari yao kabla ya kuanza safari barabarani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu