Tume ya haki za binadamu nchini Ethiopia imesema kuwa watu takribani 700 wameuawa mnamo miezi 16 iliyopita kutokana na ghasia zilizoibuka nchini humo.
Uchunguzi wa tume hiyo umebainisha kuwa wengi wao waliuawa wakati wa maandamano, pale polisi walipotumia nguvu kuzima vuguvugu la upinzani lililoshamiri katika maeneo ya vijijini mwaka mmoja uliopita.
Watu wa jamii ya Oromo waliandamana katika jimbo lao na pia katika mji mkuu, Addis Ababa, wakilalamikia kutengwa katika shughuli za kisiasa na za kiuchumi. Sheria ya hali ya hatari ya miezi sita ilitangazwa mwezi Oktoba nchini Ethiopia.
