Waziri Maghembe akiri ni kweli Faru Fausta anatumia Chakula cha Sh. Mil. 768 kwa Mwaka

In Kitaifa

Kama ulikuwa hujui Tambua sasa kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatumia Kiasi cha Shilingi Million 768 kila  mwaka kwa ajili ya kumtunza Faru Fausta katika hifadhi ya Ngorongoro.

Hayo yametanabaishwa na Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema) ambapo alitamani kujua Serikali ina mpango gani na Faru huyo.

“Hifadhi ya Ngorongoro inatumia gharama kubwa ikiwa ni pamoja na kumtunza na kumlisha chakula Faru Fausta kiasi cha Sh 64 milioni kwa mwezi, je serikali ina mpango gani kuhusu huyu Faru Fausta,” amehoji Gekul.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alikiri kuwa ni kweli mnyama huyo anatunzwa kwa gharama kubwa kwa sababu ni mzee, hivyo ananyemelewa na magonjwa mbalimbali.

Waziri alitaja sababu ya kufanya hivyo kutokana na ukweli kuwa wanyama wa aina hiyo ni wachache katika hifadhi, akasema utafiti unafanyika na kufanya ukweli wa gharama kuwa mdogo kulingana na thamani inayopatikana.

Gharama hizo zilisababisha Mbunge Frank Mwakajoka kuomba mwongozo wa spika akisema: “Majibu ya waziri anasema Faru Fausta yupo na anatunzwa kwa Sh 64 milioni kwa mwezi hii tafsiri yake anatunzwa kwa Sh 768 milioni kwa mwaka, anatoa sifa eti kwa sababu ni mzee sana, naomba mwongozo wako kuhusu hili kwa sababu mnyama huyu hawezi kuigiza faida yoyote.”

Akitoa mwongozo wake Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema suala hilo analiachia wizara na wakalifanyie kazi.

Awali katika swali lake la msingi Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya alitaka kujua serikali ina mpango gani endelevu wa kuhakikisha hadhi ya hifadhi hii inabaki kwenye ubora wake kwa ajili ya vizazi vya leo na vijavyo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema ni kweli hifadhi ya Ngorongoro ni muhimu na ina hadhi ya kipekee inayotokana na uwingi na ubora wa vivutio vyake ambavyo vinatambulika kitaifa na kimataifa.

Amesema kutokana na sifa hizo Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO kupitia orodha yake ya maeneo ya urithi wa dunia limelipatia eneo hilo hadhi yya kimataifa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu