Hakika Mtandao Namba moja Duniani kwa Kutumiana Jumbe na Mafaili mbalimbali, WhatsApp wameamua kwamba Airtel Money, M-Pesa na Tigo Pesa Wajipange kupoteza Wateja.
Wamiliki wa WhatsApp wameamua Kumuajiri Mkurugenzi mpya ambaye ataongoza jitihada hizo za malipo ya dijitali Duniani wakianza na Nchi ya India ambapo wanaamini ndipo walipo na Watumiaji WhatsApp wengi zaidi ya Nchi zote Duniani.
WhatsApp Wamesema Huduma yao hiyo mpya itashirikiana na mabenki katika kusaidia miamala ya kidijitali kwa kutumia WhatsApp. India ina watumiaji wa WhatsApp milioni 200 kila mwezi ambayo ni moja ya tano ya watumiaji wake wote ndiyo sababu ya wao kuamua Kuipeleka huduma hiyo nchini humo kabla ya sehemu zingine.
