WHO: Aina mpya ya virusi vya Covid-19 vyabainika katika nchi 17

In Kimataifa

Shirika la Afya duniania WHO limesema aina ya virusi vya corona ambavyo vinahofiwa kuchangia wimbi la visa vya maambukizi nchini India vimebainika katika mataifa mengine kadhaa duniani.Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kirusi aina ya B.1.617 vya Covid-19 ambavyo kwa mara ya kwanza viligundulika India, kwa rekodi za jana vilibainika katika mataifa mengine takribani 17. Taarifa hiyo ilisema idadi kubwa ya visa vyake vya maambukizi vimetokea Uingereza, Marekani na Singapore. Kwa namna inavyiotambulishwa aina hiyo ya virusi inaonesha kuwa ni hatari zaidi kuliko ile ya awali ikioneshwa kuwa na uwezo wa kuwa na kasi ya maambukizo au kuweza kukwepa kinga za chanjo.Mripuko wa maambukizi wa India kwa rekodi za jana pekee umesababisha visa vipya 350,000, hali inayosababisha rekodi mpya ya maambukizo duniani kufikia watu milioni 147.7 na vifo zaidi ya milioni 3.1.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu