Yuro bilioni moja Hasara kwa Man U

In Kimataifa, Michezo

Manchester United wamepata hasara kubwa zaidi katika uhamisho barani Ulaya katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kulingana na taasisi ya utafiti yenye makao yake makuu nchini Uswizi, CIES Football Observatory.

Tangu mwaka 2012 United imepata hasara kubwa ya zaidi ya euro bilioni moja, zaidi ya wapinzani wao Manchester City.

Utafiti huo umebaini kuwa Red Devils wametumia euro 1.545bn kwa ajili yauhamisho, na kurejesha euro 470m kupitia kuuza wachezaji.

Vilabu 14 vya Premier League viko kwenye nafasi ya 20 bora. United walivunja rekodi ya uhamisho wa Ligi Kuu ya Uingereza walipomsajili Paul Pogba mnamo mwaka 2016 kwa pauni milioni 89.5 na wamejipanga kutomuuza kiungo huyo wa kati, ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu.

Wachezaji wengine ambao usajili wao uliokuwa wa gharama ya juu ni pamoja na Anthony Martial (£36m) mwaka wa 2015 na Donny van de Beek (£40m) mwaka wa 2020. Wachezaji wote wawili waliondoka kwa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari.

Mabingwa wa Ligi ya Premier City wanashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na utumizi mbaya wa euro 984m.

City wametumia euro 1.699bn kununua wachezaji katika muongo mmoja uliopita lakini walifanya mauzo ya 715bn.

Paris St-Germain walikuwa wa tatu kwa orodha ya waliopata hasara ya euro 914m na Barcelona wa nne na 650m.

Arsenal ilikamilisha tano bora kwa kupata hasara ya 583m.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL) na Tanzania Red Cross Society kushirikiana kuimarisha usalama wa bodaboda 1600, kujenga jamii salama

Dar es Salaam, Tanzania. Kampuni ya TBL kupitia kampeni yake ya Cheers to Moderation, imesaini hati ya makubaliano na Tanzania Red Cross Society kwa lengo la

Read More...

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu