ZIFAHAMU HAKI ZA MKE

In Mahusiano

Kama iliyoelezwa hapo awali kwa mujibu wa akili na kwa mujibu wa sheria za Kiislamu,
mwanamme ndiye anayewajibika kwa ajili ya kumgharimia na kumtafutia mahitaji yote
ya mke wake, na katika mtazamo huu wa uwajibikaji ambao upo katika mapenzi.
Inaonekana kutoka juu kuwa chochote kile anachotaka mwanamke kwa ajili ya utulivu
wa akili yake kuwa bora kiroho, na kuridhika na mahitajio yake, vinaweza
kutenganishwa katika makundi mawili:

  1. Mapenzi halisi
  2. Kutizamwa vyema

Lau mtu atakaa kupitia orodha ya madai ya wale wenye kutetea ukombozi wa
wanawake, basi utagundua kuwa haki hizo zote ambazo zinakubaliana kiakili utaona
yako katika makundi haya mawili.
Islam imewaamrisha kwa kuwasisitiza wanaume kuwapa uhuru wake zao kufurahi haki
zao bila ya kubugudhiwa vyovyote vile. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:
“Mwanamke yeyote atakayembughudhi mume wake kwa ulimi wake….atakuwa ni wa
kwanza kuingizwa Jahannam. Na, vivyo hivyo, iwapo bwana wake hatamfanyia haki.”
Mapenzi na baraka
Imam Ja’afer Sadiq a.s. amesema:
“Mimi nina uhakika kuwa mtu anapokuwa bora zaidi katika imani na Islam basi vivyo
hivyo mapenzi ya wake zake inavyozidi.
Aya isemayo: Allah swt ameweka mapenzi na huruma baina yenu, inaonyesha kuwa
mapenzi ya kindoa ni baraka za Allah swt; na vile mtu atakavyokuwa na imani zaidi
katika Allah swt, ndivyo vivyo rehema na baraka zaidi za Allah swt zitakuwa juu ya jozi
hiyo (yaani bibi na bwana ).
Na kwa sababu hii Imam Ja’afer Sadiq a.s. amesema:”Miongoni mwa desturi za Mitume
ni mapenzi ya wanawake.”


Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema, “Ijulikane mtu bora miongoni mwenu ni yule
ambaye ni bora kwa wake zake na mimi ni bora kwa wake zangu.”
Vivyo hivyo ameendelea kusema: “Rehema na baraka za Allah swt ziwe juu ya mtumwa
wake ambaye anawafanyia wema baina yake na mke wake kwa hakika, Allah swt
amempa mamlaka zaidi juu ya mke wake na kwamba amemfanya awe ni mtu mwenye
kumhifadhi mke wake.”
Kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, imesisitizwa kuwa mwanamme anapokuja nyumbani
aje na uso wenye bashasha, mchangamfu. Nyumba hiyo itakuwa ni Jannah iwapo
sheria kama hizi zitafuatwa kwa makini.
Haki za kutimiza
Katika aya za Qurani, Allah swt anawaambia wanaume kuwatendea wema wake zao.
Mbali na aya hiyo ya hapo juu ipo aya nyingine inayosema: sura An-Nisaa, 4: 19 “…Na
kaeni nao kwa wema …”


Kuwatendea wema kwa mujibu wa Hadithi inamaanisha kuwa kile ambacho atapatiwa
mwanamke, kwa kiasi kinachowezekana, hali na desturi alivyokuwa akiishi katika
majumba ya wazazi wake; ili kwamba asipate kukabiliana na hali ya kutoishi kwa raha
na vile vile asipate ugumu wa kupata magonjwa ya akili kwa sababu ya kukosa raha
katika majumba ya mabwana zao.
Na iwapo bwana, kwa sababu za uchumi wake kuwa kiasi,anashindwa kumpatia hali
hiyo bora basi hawezi kulaumiwa.

Qurani Tukufu inatuambia katika sura Al-Baqarah 2: 236
“… Mwenye wasa’a kadiri awezavyo,na mwenye dhiki kadiri awezavyo…”
Imam Ja’afer Sadiq a.s. anatuambia: “Wale wote wanaomtegemea bwana ni wafungwa
wake, na mtumwa wa Allah swt aliyebora kuliko wote mbele ya macho ya Allah swt ni
yule ambaye anawatendea wema wafungwa wake.”
Vivyo hivyo Imam Musa al-Kadhim a.s amesema: “Wale wote wanaomtegemea
mwanamme ni watumwa wake. Kwa hivyo iwapo Allah swt anamjalia baraka zake mtu
yeyote, basi itambidi na yeye aitumie zaidi kwa ajili ya wafungwa wake; na lau
hatafanya hivyo, basi neema na baraka hiyo itatoweka”.
Kwa mujibu wa Shariah za Kiislamu, malipo, matumizi au posho ya mwanamke ni
malipo ya utiifu wake. Iwapo huyu mwanamke hamkatalii mume wake haki zake, basi
ana haki zake zote za kuruzukiwa. Iwapo bwana, kwa sababu ya matatizo yake ya
kiuchumi, anashindwa kumtimizia posho na ruzuku za mke wake, basi atabakia na deni
hilo akidaiwa na mke wake; na hivyo itambidi kumlipa mara moja pale apatapo mapesa
n.k. Kwa kifupi kumtimizia mwanamke haja zake ni juu ya misingi nipe na nikupe, na
mwanamme itambidi alipe kwa hali yoyote ile. Imam Ja’afer Sadiq a.s.
amesema: “Amelaaniwa yule mwanamme ambaye hawajali wale wanaomtegemea.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

NIFFER NA CHAVALA WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaachia huru leo mchana vijana Jennifer Jovin (26), maarufu kama

Read More...

Trump kukutana na viongozi wa Rwanda na DR Kongo Alhamisi

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Alhamisi

Read More...

SERIKALI YAAGIZWA KUFUTWA KWA LESENI 73.

Serikali kupitia Wizara ya Madini imeielekeza Tume ya Madini kufuta jumla ya leseni 73ambazo maeneo yake hayajaendelezwa. Hayo yameelezwa leo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu