SACP Fortunatus Musilimu amefanya ziara ya kushtukiza Kituo Kikuu cha Mabasi.

In Kitaifa

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu amefanya ziara ya kushtukiza Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani, Ubungo na kuzindua uwekaji wa namba za simu kwenye mabasi kwa ajili ya abiria kutoa taarifa pale madereva wanapokiuka sheria za Usalama barabarani.

Kamanda Musilimu ameeleza kuwa hatua hiyo ni kusaidia abiria kutoa taarifa pindi madereva wanapokiuka sheria za Usalama Barabarani na kuhatarisha maisha yao, na kusema zoezi hilo ni la nchi nzima ambalo litakuwa endelevu na ukaguzi wa mara kwa mara utafanyika kuhakikisha namba hizo hazitolewi kwenye mabasi hayo.

Lakini pia Kamanda Musilimu ametoa onyo kali kwa madereva na makondakta watakao ziondoa namba hizo katika mabasi, kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwaasa kuziacha namba hizo katika mabasi yao ili wasafiri waweze kuzitumia.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu