Waziri wa Elimu apiga marufuku shule ambazo azijakamilika kupewa kibali.

In Kitaifa
Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na mafunzo ya ufundi Mh. Profesa Joyce Ndalichako amepiga marufuku shule ambazo hazijakamilika na kupewa kibali kupokea wanafunzi huku akitoa mwezi mmoja kwa shule ya sekondari Mwandiga wilayani Kigoma kukamilisha miundombinu ya shule hiyo ili ipokee wanafunzi wa kidato cha tano.
Mh Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shule ya sekondari Mwandiga ambayo inatarajiwa kupokea kwa mara ya kwanza wanafunzi wa sayansi 143 wa kidato cha tano.
Hata hivyo profesa ndalichako ambapo ameagiza idara ya ukaguzi kufanya ukaguzi na kutoa kibali kabla shule kupokea wanafunzi hao.
Mapema Mkuu wa shule ya sekondari Mwandiga Albert Mutwe amesema  kuwa shule hiyo inakabiliwa naukosefu wa huduma ya maji,bwalo, usafiri, nyumba za walimu na maktaba ya shule hiyo.
Naye  mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga akiahidi kukamilisha miundombinu ya shule hiyo ili wanafunzi waweze kuanza kidato cha tano.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu