Mvua zinazoendelea kunyesha zaleta Balaa

In Kimataifa

Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali Duniani zimeleta Madhara makubwa katika mji wa Edgecumbe uliopo kaskazini mwa nchi ya New Zealand.

Maelfu ya wakazi wameyakimbia makazi yao baada ya mafuriko makubwa yaliyozunguka mji huo kutokana na mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga cha Debbie kuyafunika makazi yao.

Kimbuka hicho pia kiliiathiri nchi ya Australia Alhamisi ya wiki iliyopita na kusababisha mito mbalimbali katika nchi hiyo kujaa kingo zake.

Katika mji wa Edgecumbe maji yanasemekana kufika hadi mita 2 katika baadhi ya maeneo. Hata hivyo hakuna ripoti yoyote ya kifo katika mafuriko hayo lakini kuna mtu mmoja ambaye alikuwa katika mto ndio anatafutwa na mpaka sasa hajaonekana.

Polisi katika mji huo wamesema watapiga doria katika maeneo yaliyohamwa na kuweka vizuizi kuwazuia raia wasije wakarudi. Tazama picha za mafuriko katika mji huo hapa chini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu