Leo April 6, Shirikisho la soka Duniani, FIFA Tanzania limetangaza Viwango vyake vya mataifa katika Soka kama jadi yake ya kila mwisho wa mwezi.
Katika Viwango vyake vya mwezi uliopita ambavyo vimetangazwa leo, Tanzania imepanda kwa nafasi 22 juu.
Tangazo la mwisho lililotolewa na FIFA, Tanzania ilikuwa nafasi ya 157 na sasa imepanda nafasi 22 na kuwa nafasi ya 135 katika Dunia.
Nafasi 22 ilizovuka Tanzania huenda zikawa zimechangiwa na Mechi mbili za Kimataifa ambapo Mwezi march Tanzania ilicheza na Burundi na kushinda kwa goli 2-1 na mechi ya pili Tanzania ikacheza na Botswana na Kushinda kwa bao 2-0.
Viwango hivi vimeifanya Burundi kushuka Kiwango kutoka nafasi ya 139 hadi nafasi ya 141 Lakini pia Botswana Wameshuka kutoka nafasi ya 116 hadi nafasi ya 120.
