Watu 6,529 Wamefariki kwa ajali za Bodaboda Nchini

In Kitaifa

Bado Ajali za Bodaboda ni Kisababishi cha Maelfu ya Vifo Nchini.

Serikali imesema watu 6,529 wamefariki dunia huku watu 30,661 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na ajali 31,928 zilizosababishwa na pikipiki maarufu bodaboda na bajaji katika kipindi cha miaka saba kati ya Januari 2010 hadi Februari 2017

Akijibu swali la mbunge Abdallah Haji Ali wa jimbo la Kiwani, aliyeuliza ni watu wangapi wamepoteza maisha na wangapi wamejeruhiwa kwa ajali za bodaboda kuanzia mwaka 2010 hadi 2017.

Waziri wa mambo ya ndani, mheshimiwa Mwigulu Nchemba, amesema usafiri wa bodaboda na bajaji ulianza mwaka 2008, lakini serikali ilipitisha kanuni na masharti ya usafirishaji mwaka 2010, lakini hakuwa na utaratibu wa kusimamia biashara hiyo.

Mheshimiwa Nchemba amesema kipindi cha Januari 2010 hadi Februari 2017, kumekuwa na jumla ya ajali 31,928 zilizosababisha vifo vya watu 6,529 na majeruhi 30,661.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MABELE AHITIMISHA MAFUNZO YA JKT KWA VIJANA

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya

Read More...

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu