Bado Ajali za Bodaboda ni Kisababishi cha Maelfu ya Vifo Nchini.
Serikali imesema watu 6,529 wamefariki dunia huku watu 30,661 wakiwa wamejeruhiwa kutokana na ajali 31,928 zilizosababishwa na pikipiki maarufu bodaboda na bajaji katika kipindi cha miaka saba kati ya Januari 2010 hadi Februari 2017
Akijibu swali la mbunge Abdallah Haji Ali wa jimbo la Kiwani, aliyeuliza ni watu wangapi wamepoteza maisha na wangapi wamejeruhiwa kwa ajali za bodaboda kuanzia mwaka 2010 hadi 2017.
Waziri wa mambo ya ndani, mheshimiwa Mwigulu Nchemba, amesema usafiri wa bodaboda na bajaji ulianza mwaka 2008, lakini serikali ilipitisha kanuni na masharti ya usafirishaji mwaka 2010, lakini hakuwa na utaratibu wa kusimamia biashara hiyo.
Mheshimiwa Nchemba amesema kipindi cha Januari 2010 hadi Februari 2017, kumekuwa na jumla ya ajali 31,928 zilizosababisha vifo vya watu 6,529 na majeruhi 30,661.
